Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-
Dar es Salaam, Tanzania - Mashindano ya Kisayansi na Kimataifa yaliyoshirikisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya kidini na vya kisekula yalifanyika Kibaha Siku ya Jumapili tarehe 12 Oktoba 2025, yakijikita katika Maudhui tofauti za utafiti wa kielimu na kisayansi kama vile:
1_Uchawi kwa mujibu wa mtizamo wa Qur'an na Sunna. 2_Uchambuzi wa Aya za Qur’an Zinazozungumzia Uchawi (mfano: Surah Al-Baqara 102).
3_Uchawi katika Hadithi Sahihi: Uchambuzi na Uhalisia Wake.
4_Uchawi katika Muktadha wa Tamaduni za Kiafrika na Mtazamo wa Kiislamu.
5_Mchango wa Watafiti wa Kiislamu katika Kueleza Ukweli wa Uchawi.
6_Ulinganifu kati ya Mitazamo ya Kiislamu na Kisaikolojia kuhusu Uchawi.
7_Uchawi na Ulimwengu wa Ghaibu: Uelewa wa Kiislamu.
8_Athari za Imani ya Uchawi katika Maendeleo ya Jamii za Kiislamu.
9_Misingi ya Kiakida katika Kupinga Imani za Uchawi**
10_Jukumu la Elimu ya Dini katika Kupunguza Imani za Kishirikina.
11_Uchawi na Teknolojia ya Kisasa: Je, kuna uhusiano?.
Taasisi na vyuo vinne vilishiriki katika mashindano hayo, ikiwemo Taasisi ya Kimataifa ya Al-Mustafa (s). Wanafunzi wavulana wa Chuo cha Al-Mustafa - Mbezi Beach waliwakilisha taasisi yao kwa umahiri mkubwa na hatimaye wakaibuka washindi wa nafasi ya pili katika mashindano hayo.
Ushindi huu unaonyesha kiwango cha juu cha ubunifu, juhudi, na umahiri wa kielimu wa wanafunzi wa Al-Mustafa (s) katika nyanja ya utafiti wa kisayansi na kijamii.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) linawapongeza kwa dhati wanafunzi hao kwa ushiriki wao mzuri na mafanikio yenye athari chanya katika kukuza elimu na utafiti wa kisayansi nchini.
Your Comment